Katika kilimo, si kila mimea huishi vizuri ikipandwa karibu na mingine. Baadhi ya mimea hushindania virutubisho, huzuia ukuaji wa mingine, au huvutia wadudu na magonjwa yanayodhuru mazao jirani.
Kujua ni mimea ipi haifai kupandwa pamoja husaidia
kuongeza mavuno na kuboresha afya ya udongo.
Hii hapa ni orodha ya mimea 10 ambayo hupaswi kuipanda
pamoja:
1. Mahindi na nyanya
Mahindi huvutia wadudu kama funza wa mahindi ambao pia
hushambulia nyanya. Pia mahindi hurefuka na kuzuia mwanga wa jua kufika kwenye nyanya.
2. Viazi mviringo na nyanya
Nyanya na viazi hutoka familia moja (Solanaceae),
hivyo hushambuliwa na magonjwa yanayofanana yakiwamo ya bakiteria na fangasi.
Kupanda pamoja huongeza hatari ya maambukizi.
3. Bizari (dill) na karoti
Bizari inapokomaa huathiri vibaya ukuaji wa karoti na
inaweza kuzuia ukuaji wa mizizi yake.
Dill
4. Maharage na vitunguu
Vitunguu hutoa kemikali asilia zinazozuia ukuaji wa
maharage, hivyo mazao haya mawili hayafai kupandwa karibu.
5. Kabichi na nyanya
Nyanya huzuia ukuaji wa kabichi, na pia mimea hii
huvutia wadudu tofauti wanaochochea kuathiriana.
6. Tango na viazi
Viazi huvutia magonjwa ya majani ambayo yanaweza
kuambukiza matango, na pia hupunguza nafasi ya ukuaji wa matango.
7. Maharagee na kitunguu saumu
Kitunguu saumu, kama vitunguu maji, hupunguza ukuaji
wa maharage kutokana na kemikali zake kali.
8. Hoho (Pilipili hoho) na Maharage
Maharage huathiri vibaya ukuaji wa hoho kwa
kushindania virutubisho na maji.
9. Tikiti maji na viazi
Viazi huongeza hatari ya magonjwa ya udongo ambayo
yanaweza kushambulia tikiti maji.
10. Mbaazi na vitunguu
Kama ilivyo kwa maharage, mbaazi hazistawi vizuri
zikipandwa karibu na vitunguu.
Hitimisho
Kupanda mimea inayofaa pamoja (companion planting) ni
mbinu muhimu ya kilimo endelevu. Epuka kupanda mimea inayopingana, kwa kufanya
hivyo utalinda afya ya mazao yako, kupunguza matumizi ya dawa na mbolea na
kuongeza mavuno.
Pamoja na kwamba nimeanza kueleza mimea isiyofaa
kupandwa pamoja, nakuletea pia orodha ya mimea inayofaa kupandwa pamoja
1. Nyanya
Hufaa kupandwa na:
Basil (mvumbasi) – hufukuza wadudu na kuboresha ladha.
Pia unaweza kupanda na vitunguu maji, vitunguu saumu, karoti na marigold (ua ya
mapambo)
2. Mahindi
Hufaa kupandwa na:
Maharage ambayo husaidia kurejesha nitrojeni kwenye
udongo na maboga. (mfumo huu hujulikana kama “Dada watatu” – Three Sisters)
3. Maharage
Hufaa kupandwa na:
Mahindi, karoti, kabichi, matango
4. Kabichi na jamii yake
(Inajumuisha kabichi, broccoli, cauliflower)
Hufaa kupandwa na:
Vitunguu, kitunguu saumu, celery na ua aina ya marigold
linalosaidia kufukuza wadudu waharibifu.
5. Karoti
Hufaa kupandwa na:
Vitunguu, nyanya, maharagwe na leeks
6. Matango
Hufaa kupandwa na:
Maharage, mahindi, bizari (ikiwa changa) na radish.
7. Pilipili (Hoho na Pilipili Kali)
Hufaa kupandwa na:
Vitunguu, basil, nyanya na marigold
8. Viazi
Hufaa kupandwa na:
Maharage, kabichi na mahindi
Horseradish
9. Maboga
Hufaa kupandwa na:
Mahindi, maharage na radish
10. Lettuce (Saladi)
Hufaa kupandwa na:
Karoti, matango, radish na vitunguu
Faida za kupanda mimea inayofaa pamoja ni pamoja na kuongeza
rutuba ya udongo, kupunguza wadudu waharibifu, kuhifadhi unyevu wa udongo na kuongeza
mavuno.
PICHA ZOTE NA PINTEREST




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni