Jumamosi, 13 Aprili 2026 · Dar es Salaam, Tanzania
kijijichetumedia.com
Kijiji cha Habari Media
Kijiji cha Habari Media Simulizi za Mageuzi · SDGs · Tanzania
LEO
Fugakuku Business Solution yafunza wafugaji 2,000+ Tanzania — Soma simulizi yake hapa    •    Fugakuku Business Solution yafunza wafugaji 2,000+ Tanzania — Soma simulizi yake hapa    •   

Jumanne, 5 Agosti 2025

Jinsi ya kuanzisha bustani ya mboga nyumbani kwa kutumia matairi, chupa, makopo ya maua

 

UWE kwenye nyumba ya kupanga au ya kwako uliyoijenga mwenyewe, unaweza kabisa kula mboga za majani zilizo ‘fresh’, salama na zenye afya.

Mtaalamu wa bustani, Janeth Augustino, anasema ni rahisi kuanzisha bustani ya mboga za aina mbalimbali nyumbani kwa kuwa ni mimea inayohitaji mwanga na jua kiasi, hali ambayo unaweza kuikabili kwa kufanya ubunifu kidogo.

Anasema tairi chakavu au chupa za maji ya kunywa, ni zana nzuri za kuanzisha bustani ya mboga nyumbani.

Kwa mfano wakati wa mvua, mboga huwa zinaadimika sana kwa sababu nyingi zinalimwa kwenye mashamba makubwa ambako mkulima hawezi kuzuia hali ya hewa, ukiwa na bustani ya matairi kibarazani, unaweza kuzisogeza juani na kuzifanya zishamiri, wakati wa jua unazikinga kwa kuziacha kibarazani muda mwingi,” anasema.

Janeth anasema tairi chakavu, viroba, chupa za plastiki au makopo ya kupandia maua yanaweza kutumika kutengeneza bustani hiyo ya mboga.

Anasema: “Kwa wanaotaka kutumia vibaraza, matairi au makopo ni mazuri zaidi kwao, wanaoweza kutumia viroba wanatalazimika kuviweka chini pembeni ya uzio au nyumba, ni bustani nzuri inayokuhakikishia usalama na ubora wa mboga unazokula.”

Anasema bei ya mbegu ya mchicha na aina nyingi za mboga inaanzia Sh. 500 na kwamba kwa bustani ndogo za vibarazani, mbegu za Sh. 500 zinatosha kwa kuanzia.

Anashauri kwamba bustani hizo hazihitaji kupulizwa dawa za kemikali na badala yake, majivu au maji ya majani ya mwaobaini yaliyochemshwa yanaweza kutumika kama kiuatilifu salama.


"Unaweza pia kutumia vinegar kwa kuichanganya na maji, ukapuliza kwa ajili ya kuzia ukungu sio tu kwenye mboga, bali kwenye mimea mingine kama miti ya matunda mfano mpera au mwembe...hii inatumika kidogo sana, kwenye maji lita 20," anasema. 

Anasema mkulima anaweza kutengeneza bustani ya vitunguu, matango, matikiti, pilipili, viungo kama rosemary na mint pamoja na aina mbalimbali za mboga.


Picha zote na PINTEREST.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni