Picha za hivi karibuni kuhusu mapambo ya ndani zinaonesha ubunifu wa holder za mishumaa na taa, ambazo zimebuniwa kisasa kwa mwonekano wa kizamani; ambao unaongeza ‘ladha’ ya kipekee ndani ya nyumba.
Holder hizi zinaweza kutengenezwa kwa chuma, udongo au mbao kwa maumbo tofauti tofauti ikiwamo michoro ‘tata’ kama iliyopo kwenye mapango ya kale, wanyama, watu au kitu chochote kulingana na uwezo wa mbunifu.
Ni kitu kizuri sana kuwa nacho nyumbani lakini pia unaweza kumpa rafiki zawadi kwenye tukio lake maalumu; haipitwi na wakati na inaeleza historia fulani ya maisha. Mfano, holder yenye wanawake wamebeba vyungu, inaeleza aina ya maisha ya wanawake wa Kiafrika.
Ni ubunifu unaoongeza mwonekano mzuri ndani ya nyumba, kwani hata kama mtu hahitaji kuwasha mshumaa kila wakati, holder hiyo inaweza kutumika kama pambo.
Pengine unajiuliza ni wapi unaweza kuiweka. Kwenye meza ya chakula, sinki la kunawia, console au ya kahawa. Kwa wenye madirisha yenye nafasi ya kuweka mto, holder hii ni mahali pake. Ukiwa hujawasha mshumaa inabakia kuwa pambo sehemu ilipo.
Picha zote na PINTEREST






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni