Jumamosi, 13 Aprili 2026 · Dar es Salaam, Tanzania
kijijichetumedia.com
Kijiji cha Habari Media
Kijiji cha Habari Media Simulizi za Mageuzi · SDGs · Tanzania
LEO
Fugakuku Business Solution yafunza wafugaji 2,000+ Tanzania — Soma simulizi yake hapa    •    Fugakuku Business Solution yafunza wafugaji 2,000+ Tanzania — Soma simulizi yake hapa    •   

Jumatatu, 4 Agosti 2025

Sebule rafiki kwa mazingira: Mapambo ya nyumba yanavyosaidia kupunguza msongo wa mawazo uwapo nyumbani


TUNAPOWAZA kuhusu utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kuokoa dunia, fikiria pia eneo dogo la nyumba yako na uwaze kupafanya mahali pa kupumzika na rafiki kwa mazingira, ili kukuza utulivu na afya njema kwa familia.

Ukiwaza hivi, utatengeneza sebule yenye mzunguko mkubwa wa oksijeni, ili kufurahia mazingira ya nyumbani ambayo sio tu maridadi, lakini pia yanayofaa kwa afya yako ya akili na sayari yetu.

Mtaalamu wa mapambo, Lugano Nsebo, anasema mazingira asilia yanasaidia mtu awapo nyumbani aweze kupumzika eneo lenye hewa safi na kuboresha afya kwa ujumla.

“Mimea hasa inayozalisha hewa safi kwa wingi inakufanya uwapo sebuleni kwako uvute oksijeni na kukusaidia kurejesha utulivu kwenye mishipa yako ya fahamu kutokana na mzunguko mkubwa wa hewa hiyo. Ni mchanganyiko wa maisha bora na usafi kwa ujumla,” anasema.

Anasema mimea inaifanya nyumba iwe kisiwa cha maisha safi, akishauri inapendeza zaidi kama vitu vingine kama samani na kazi za mikono zitatumika na picha mbalimbali ndani ya nyumba.

“Ili sebule yenye maua ndani ivutie ni muhimu kuipanga kimkakati kuanzia rangi, samani, picha za ukutani na taa,” anafafanua.

Lugano anasema kitu kingine cha kuzingatia ni mito ya kwenye sofa, seti ya televisheni na muziki, zulia na mwanga asilia wa jua au mwezi kupitia dirishani.

Anasema ipo mimea inayofaa kwa ajili ya kupanda ndani ikiwamo ulimi wa mama mkwe (snake plants), ua la amani (peace lily) na mingine inayozalisha kwa wingi hewa safi ya oksijeni nyakati zote.

Hata hivyo, anasema mimea isiyo asilia (artificial plants), kama mitende, inaweza kuwekwa pamoja na mimea asilia na kuongeza uasilia ndani ya nyumba.


PICHA ZOTE NA PINTEREST.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni