KUWA na bustani ya nyumbani yenye kivuli na mandhari tulivu ni njia bora ya kuongeza uzuri na utulivu kwenye makazi yako.
Bustani
hizi si tu kwamba huongeza thamani ya nyumba, bali pia hutoa nafasi ya
kupumzika, kushiriki chakula cha familia, au kupokea wageni kwa starehe. Kwa
kutumia vifaa vya gharama nafuu kama mbao, chuma na makuti, unaweza kuunda
kijumba kizuri cha bustani chenye kivuli cha asili.
Hili limerahisishwa zaidi kutokana na matumizi ya teknolojia,
ambapo kupitia
mitandao ya kijamii, sasa ni rahisi zaidi kujifunza mbinu za kutengeneza
bustani za kisasa nyumbani kutoka kwa wabunifu wa ndani na nje ya nchi.
Aidha, unaweza kutengeneza eneo hili muhimu nyumbani na
kwa gharama
nafuu, kupitia ubunifu ambao umerahisishwa kutokana na namna ambavyo
matumizi ya teknolojia na upatikanaji wa habari, unavyotoa nafasi ya
kujifunza kutoka kwa wabunifu wa wataalamu wa nyumba kwa urahisi kabisa.
Ipo mitandao na tovuti mbalimbali zinazotoa fursa ya watu kuona kazi za maboresho ya nyumba kuanzia ujenzi hadi ukamilishaji na mazingira yake.
Wabunifu mbalimbali wanasema kijumba binafsi kina faina nyingi
ikiwamo kupamba bustani au eneo la nyumba, kwa kuhakikisha kivuli kipo muda
wote na hivyo kuwa na mazingira ya kupumzika kila wakati.
Ni eneo zuri kwa ajili ya mazungumzo ya familia na hasa siku za mapumziko kupata chakula pamoja au kinywaji.
Ni
sehemu inayoweka kumbukumbu za kifamilia na ni eneo zuri sana kukaa na mgeni.
Ukiwa na kivuli cha aina hii, hutotamani kutoka nyumbani, kwa
ujumla, ni sehemu ambao inapaswa kujengwa katika kila nyumba.
Aidha, malighafi za kujenga kijumba hichi,
zinapatikana kulingana na mtazamo wa mwenye nyumba, kwa kuwa kinaweza
kutengenezwa kwa chuma na mbao au mojawapo ya zana hizo, ikiezekwa kwa bati au makuti;
kulingana na pendekezo la mwenye nyumba.
Kwa kazi nzuri zaidi, unaweza kumtumia mtaalamu wa
nyumba au kutafuta mfanano mtandaoni na kujionea
aina mbalimbali kabla hajafanya maamuzi ya ujenzi.
DONDOO MUHIMU
·
Kinapendeza kikijengwa kwa mbao.
·
Panda maua machache kukizunguka.
·
Unaweza kuweka mapazia, mlango sio lazima.
·
Fenicha za nje za asilia ni nzuri zaidi.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni