NYUMBA iliyopangwa vizuri inaweza kuokoa muda, kupunguza msongo wa mawazo na kuhamasisha kukaa ndani hasa maeneo muhimu kama jikoni.
Nikianzia jikoni,
mpangilio utakupa mwelekeo wa kutumia nafasi kikamilifu na kuweka kila kitu
kikiwa katika mwonekano mzuri.
Jambo la msingi ni
kutengeneza shelve na kuhakikisha kila kitu kinakaa sehemu yake, kuanzia
viungo, matunda, nafaka nk, ili kuimarisha mpangilio na urahisi wa upatikanaji
wa vitu.
Utaratibu wa mpangilio
hii unakusaidia kuokoa muda na kudumisha usafi nyumbani.
Unaweza kupangilia
kuanzia ukuta kama inavyoonekana pichani na kuweka vitu vinavyofanana pamoja,
mathalani, vitunguu, viazi na nyanya.
Mbinu hii inawezesha
nyumba yako kuonekana nadhifu na pia hurahisisha upatikanaji wa vitu
unavyovitafuta kwa haraka. Kwa kuvigawa vitu kama vile vitafunwa, vifaa vya
kuokea, au bidhaa za makopo katika makundi, unaepuka msongamano na kuboresha
urahisi wa kuvifikia.
Kama bado unaweka
vitu chini, na ungetamani nyumba yako iwe na nafasi na mwonekano maridhawa,
jaribu mbinu hii inayoweza kubadilisha chumba mara moja kutoka kuwa cha kawaida
hadi kuwa mahali pa utulivu wa kibinafsi, wa kisanaa, na wa vitabu.
PICHA ZOTE NA PINTEREST



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni