Jumamosi, 13 Aprili 2026 · Dar es Salaam, Tanzania
|
kijijichetumedia.com
Kijiji cha Habari Media
Kijiji cha Habari Media Simulizi za Mageuzi · SDGs · Tanzania
LEO
Fugakuku Business Solution yafunza wafugaji 2,000+ Tanzania — Soma simulizi yake hapa    •    Fugakuku Business Solution yafunza wafugaji 2,000+ Tanzania — Soma simulizi yake hapa    •   

Jumatano, 30 Septemba 2026

Mabosi wa teknolojia wabadili jina la AI kuwa SI

 

Rais Donald Trump, akiwa na Watendaji Wakuu wa kampuni za teknolojia. Picha: AFP-KENT NISHIMURA

Vigogo wanaomiliki kampuni za teknolojia, wamekubaliana kubadili jina la Akili Unde (AI) kuwa Akili ya Juu Zaidi (Superintelligence), baada ya kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump, katika Ikulu ya White House, jijini Washington.

Rais Trump ametia saini agizo la kiutendaji baada ya kukutana na Elon Musk, Mark Zuckerberg, Mkurugenzi Mtendaji wa Nvidia, Jensen Huang, pamoja na viongozi wengine wakuu wa sekta ya teknolojia.

Kundi hilo pia lilitia saini makubaliano mapya yanayolenga kujisimamia na kujiwekea kanuni katika sekta hiyo, huku Trump akisema teknolojia hiyo imepiga hatua kubwa kiasi kwamba jina la AI halitoshelezi tena kuelezea uwezo wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Anthropic, Dario Amodei, amesema SI ina manufaa makubwa, lakini pia hatari halisi.

“Kile ambacho nimekuwa nikisema siku zote ni kwamba AI (SI), ina manufaa makubwa sana. Nimezungumzia manufaa ya teknolojia hii katika sekta ya afya, kama Rais alivyoeleza. Yeyote atakayeshinda katika AI, atashinda.”

“Sote tunapaswa kushirikiana kuhakikisha kwamba tunashinda, na tunaweza kushinda kwa usalama ikiwa tutafanya mambo haya kwa usahihi. Tukishirikiana na Rais pamoja na kila mtu aliyepo hapa, tunaweza kushinda kwa usalama.”

Chanzo: Foxbusiness

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni