![]() |
| PICHA: PINTEREST |
MIMEA ya ndani ni moja ya mapambo bora yanayoleta uhai
wa nyumba; mchawi akiwa sanaa ya kupangilia vyungu kulingana na urefu, upana na
aina ya mmea husika.
Wataalamu wa mapambo ya ndani (interior designers), wanaona
kwamba mimea ya ndani kama maua yanayoongeza hewa ndani na yanayodaka vumbi
yanaweza kuifanya nyumba yako ionekane ya kifahari na kukupa matokeo makubwa.
Je, umewahi kuingia kwenye ukumbi wa hoteli ya nyota
tano au penthouse ya mamilioni ya dola na kujiuliza: “Kwa nini eneo hili
linaonekana la hali ya juu na tulivu kwa namna ya kipekee?
Siri mara nyingi haipo kwenye sofa za ngozi ghali
kupindukia au michoro ya kibunifu ukutani; bali katika asili yaani mimea
iliyopandwa na ilivyopangiliwa.
Mimea imevuka hadhi ya kuwa pambo la ziada na kuwa kitovu
cha ufahari, kikiwa kipengele hai kinachoweza kukuza hadhi ya nyumba na kuweka
utambulisho wa kimaridadi usio na kifani.
Ili kupata mwonekano wenye hadhi ya juu, inahitaji
ubunifu wa kupanga bustani yako ya ndani kwa ustadi; ikiwezekana weka ‘msitu wa
ndani uliojaa vurugu.’
Ili kuweka hadhi hiyo, hautahitaji mimea mingi bali namna
ulivyochagua, eneo unapoyaweka na ufikiaji wa mwanga na kivuli.
Ukishajua kile unachotamani kitokee kwa kupanda mimea
ya ndani, utahakikisha kila jani linakaa mahali pake, ili kuonesha upekee wake.
Kwanza utazingatia aina ya yale ambayo ungependa yatawale (Statement Piece).
Mmea au ua liwe dogo au kubwa, kinachozingatiwa ni
matokeo ya mwonekane wake wa mwisho. Wataalamu wanashauri kwamba badala ya
kusambaza vyungu vidogo vingi ‘vinavyoweza kuchafua’ mwonekano, wekeza kwenye
mti mmoja mkubwa wenye umbo la kuvutia.
Mosi, fikiria mti
mrefu kama ‘rubber plant’ na uweke kwenye sehemu kuu ya kuvutia macho; kama pembeni
ya sofa au kona yenye mwanga mwingi wa jua.
Mti au ua refu kuelekea dari huleta hisia ya urefu wa
kimuundo na mamlaka, na mara moja hutuma ujumbe wa hadhi ya juu.
Ni bora kuwa na mti mmoja wenye afya na wa kuvutia
kuliko kumi ‘inayohangaika.
Pili, zingatia kina
na vipimo. Changanya viwango vitatu vya urefu kwa kuweka mrefu kama mhimili
(anchor), ua la ukubwa wa kati kama Snake Plant kwa muundo na dogo linaloning’inia
chini ili kuleta ulaini.
Usisahau kutmia stendi zenye ubora kama mbao iliyopigwa
msasa na polisi vizuri au chuma kilichopigwa rangi nyeusi au nyeupe, ili kuunda
ubora wa ustadi wa kitaalamu.
Tatu, chagua vyungu vya maua. Unaweza
kununua mmea mzuri kwa gharama kubwa, lakini ukiuweka kwenye chungu cha
plastiki cha bei rahisi, thamani yake hushuka. Fikiria chungu kama ‘vazi bunifu’
la mmea wako.
Katika hili, zingatia rangi zinazooana na ukuta wa
nyumba yako. Unaweza kuamua vifanane au vioane; aidha, nyeupe hafifu, kijivu
isiyokoza huipa nyumba mwonekano wa gharama kubwa.
Nne, kumbuka kwamba kila nyumba
ina sehemu ‘iliyokufa’, na mimea ndio tiba ya kufufua maeneo hayo.
Maeneo kama chini ya ngazi, korido nyembamba, au pengo
tupu karibu na kabati la pembeni; ni maeneo unayoweza kuyapa uhai kwa kuweka ua.
Kufanikisha hili, kunaleta tafsiri kwamba kila mita ya mraba imepangwa kwa
makusudi.
Kwa upande wa bafuni au chooni, weka mimea inayofyonza
unyevunyevu.
Kwenye mlango mkubwa, weka vyungu vya hadhi sawa pande
zote za mlango na upande maua kwa usanifu unaoongeza hadhi ya nyumba yako.
![]() |
| PICHA: PINTEREST |
Usisahau kitabu kwenye meza yako ya kahawa (coffe
table) au console. Hapa utachanganya na maua madogo ili kuweka uhai unaotakiwa.
HITIMISHO
Upangaji wa mimea ni sanaa kuu ya kuipa nyumba yako
utambulisho wa kipekee. Ingawa hakuna sheria zisizobadilika, kuchanganya mbinu
hizi kwa uangalifu kutabadilisha kabisa nafasi yako. Hakikisha
kila mmea ni safi bila vumbi (futa majani) kwani usafi ni mshirika kimya wa mwonekano
wa kifahari.
Kwa kufanya hivi, nyumba yako itakuwa na aura mpya,
mwonekano wa kistaarabu, mvuto na thamani isiyochuja.
Unahitaji msaada wa kupata mpangilio huo, andika maoni
yako ili kwa pamoja tushirikiane kuunda kona bora ya kijani kwa ajili yako.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni