WATAALAMU wa rangi wanakumbusha kwamba kijivu ni chaguo sahihi linalobadilika kirahisi, kutokana na uwezo wake unaorahisisha mpangilio wa mwingiliano wa rangi.
Kijivu zote kuanzia iliyokoza (dark gray), mpauko
kiasi na iliyopauka kiasi cha kuelekea kwenye weupe (light gray), ni chaguo
sahihi kuanzia kwenye uzio wa nyumba hadi vyumbani.
Wanasema inaongeza utulivu ndani ya nyumba kutokana na
kwamba unaweza kumechisha na rangi karibu zote kuanzia nyeupe, nyeusi, kijani,
nyekundu, machungwa, bluu au uzurungi.
Wanashauri kwamba ikiwa utapendelea kupaka rangi hiyo
katika chumba cha kulala, utatengeneza mazingira yenye hewa na mwanga, huku
miundo yenye rangi kali kwenye mashuka ikiongeza vipengele vya furaha na
utulivu.
Hii ni kwa sababu ya uwezo wake wa kuendana na mitindo
mbalimbali huruhusu muunganiko mzuri wa ustaarabu na faraja. Kwa kujumuisha za
vitu tofauti, mtu anaweza kuunda mazingira yenye tabaka la ufahari hasa ikiwa
nakshi nyingine ndani ya chumba kama picha zenye maandishi au mito itakuwa na
rangi inayomechisha ukuta.
Ni rangi rahisi kwa wanaopenda kubadilisha mwonekano
wa nyumba huku wakitunza tulivu maridadi.
Ili kupata mandhari yanayokusudiwa, ongeza vitu vingi vya kijivu ili kuinua mvuto wa urembo wa nafasi ndani ya nyumba.
Mathalani, kama ukuta wa chumba ni kijivu mpauko, basi inashauriwa mapambo au nakshi nyingine ziwe za kijivu kilichokolea (charcoal). Saikolojia ya rangi inaonesha kwamba kufanya hivyo kunaleta utofauti mzuri na kufanya kila kitu kionekane vizuri.
Wataalamu wanasema mpangilio huu wa chumba huunda
tabaka la uhai, huku vifaa vya asili kama mbao vikiongeza joto na kuimarisha
mvuto wa kuona kwa kina mwonekano wa chumba chote.
Kama tayari umeshapiga nyumba yako rangi, unaweza
kubadili mwonekano wa upande mmoja wa ukuta kwa kuweka ‘wall paper’ ya kijivu
kuongeza uzuri wa mtindo wowote wa mapambo.
Hii itakusaidia kupunguza ukali wa rangi, kuongeza
mvuto na utulivu.
Usisahau kuweka pazia linaloakisi hali ya utulivu.
Unaweza kutumia mito ya rangi ya waridi hafifu huku ukijumuisha pia samani za
mbao kama kitanda, kabati na sofa ambazo unaweza ‘kurushia’nakshi ya kijivu
kwenye milango ili kuongeza mwonekano wa kifahari na mandhari ya kisasa.
Unaweza kujumuisha rangi kama bluu ya kijani (teal) au
njano ya mustard, kuongeza mvuto.
Fikiria pia vyumba vya watoto ambapo kijivu hutumika
kama chaguo linalobadilika kirahisi, likiendamana na mabadiliko ya mtoto kadri
anavyokua. Kuta za kijivu hafifu huunda mazingira yenye hewa na mwanga, huku
miundo yenye rangi kali kwenye mashuka ikiongeza vionjo vya furaha.
<meta name="p:domain_verify" content="03b68c6ff6de7de06df0cf04859bccaa"/>


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni