Kuna tabia zinazoonekana kama za kawaida, ilihali zinaifanya
miili yetu kuzeeka kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Inawezekana pia kwamba
umekuwa ukiuchochea uzee kwa kuendekeza tabia hizi.
Huenda unakula vizuri, unafanya mazoezi, unalala kwa saa
7; lakini bila kujua kuna mambo unafanya kila siku yanayoathiri afya yako polepole.
Yamkini unaongeza kiwango cha homoni ya msongo
(cortisol), unavuruga uwiano wa homoni, unaharibu mmeng’enyo wa chakula, unapunguza
kasi ya urekebishaji wa seli na kuharakisha dalili za uzee kuanzia ndani ya
mwili.
Kunywa kahawa kabla ya kula unaongeza mzigo mkubwa wa cortisol
(unachochea msongo wa mawazo). Ikiwa unatumia air fresher; unahatarisha homoni.
Kama unakunywa maji ya bomba yasiyochujwa, unaongeza mzigo wa sumu mwilini.
Kama unatabia ya kula kwa haraka, unajiweka kwenye
hatari ya kuvimbiwa na tatizo sugu la gesi; kama unakula usiku sana, unaathiri
urejeshaji wa mwili wakati wa usingizi.
Aidha, kama una kula kiasi kidogo cha protini
unadhohofisha misuli na kama unakula snacks mara kwa mara unachoche kiwango cha
insulini (sukari) na pia kama unakosa mwanga wa jua unapunguza vitamini D na
hali ya hisia wakati msongo wa mawazo wa muda mrefu unazeesha ngozi na ubongo.
Upungufu wa magnesiamu kunakakamaza misuli kukakamaa
na msongo na kunywa maji baridi pamoja na chakula kupunguza kasi ya mmeng’enyo.
1. Vyakula vyenye protini kwa wingi
Protini husaidia kujenga misuli, kurekebisha seli na
kuimarisha kinga ya mwili.
Samaki (dagaa, sato, sangara, salmoni), nyama nyekundu
(ng’ombe, mbuzi), kuku na mayai, maziwa, mtindi na jibini, maharagwe, njugu na
karanga, dengu, choroko, kunde, soya na bidhaa zake (maziwa ya soya, tofu).
2. Vyakula vyenye Vitamini D kwa wingi
Vitamini D huimarisha mifupa, meno na mfumo wa kinga.
Samaki wenye mafuta mengi (dagaa, salmoni, sato,
sangara), mayai (hasa kiini cha yai), maziwa yaliyoongezwa vitamini D, siagi na
jibini, maini, uyoga (hasa uliokaushwa au uliopata mwanga wa jua)
Kumbuka: Mwanga wa jua ni chanzo kikuu cha
vitamini D.
3. Vyakula vizuri kwa afya ya ubongo
Husaidia kumbukumbu, umakini na afya ya mfumo wa neva.
Samaki wenye mafuta mengi (dagaa, salmoni), karanga,
njugu na korosho, mbegu za maboga, alizeti na ufuta, matunda yenye rangi ya
bluu na zambarau (blueberries, zabibu), mboga za majani ya kijani kibichi
(mchicha, kisamvu), parachichi, mayai, chokoleti nyeusi (dark chocolate kwa
kiasi)
4. Vyakula vyenye magnesiamu kwa wingi
Magnesiamu husaidia misuli, neva, usingizi na
kupunguza msongo wa mawazo.
Karanga na njugu, mbegu za maboga, ufuta na alizeti, maharage
na dengu, mboga za majani ya kijani kibichi (mchicha, matembele), ndizi, parachichi,
nafaka zisizokobolewa (unga wa dona, mchele wa kahawia), kakao na chokoleti
nyeusi.
Mabadiliko madogo, manufaa makubwa katika kupambana na
kuzeeka, unavyojisikia na unavyopona. Nimekuandikia kukupa ari ya kuamka.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni