Kula kiafya si suala la kujinyima, ni kuhusu kuchagua mchanganyiko bora zaidi. Jambo la muhimu zaidi kulifahamu ni kwamba chakula chako kinaweza kufanya kazi vizuri zaidi unapofahamu jinsi kinavyoshirikiana.
Nakuletea mchanganyiko unaosaidia afya yako pindi
utakapoamua kula kwa pamoja vyakula hivi kuliko kula peke yake.
Wataalamu wa lishe wanasema kwamba berries na mtindi ni
mchanyiko unaokuwa kiwango cha juu cha antioxidants kwa ngozi ang’avu na kinga
imara.
Ukila tikiti maji na ndimu, inakupa vitamini C na maji
mengi kwa usafi wa ini na kuongeza uwezo wa mwili kujisafisha.
Mchanganyiko wa asali na mdalasini unakusaidia
kusawazisha homoni na kupunguza uvimbe mwilini.
Ukila mchanganyiko wa beetroot na chungwa, unapata mzunguko
bora wa damu na kuongeza nguvu asilia.
Chai ya kijani (green tea) na limau inasaidia kuchoma
mafuta kwa kasi na ulinzi wa kinga; wakati tango na mnanaa unasaidia kutoa sumu
mwilini.
Ukila tofaa na siagi ya karanga kinakuwa kiwango
thabiti cha sukari kwenye damu na nishati safi, broccoli na mafuta ya mizeituni
unaupa mwili wako urahisi wa ufyonzwaji wa virutubisho na uimarishaji wa afya
ya moyo.
Ukila ndizi mbivu na mbegu za chia inaimarisha afya ya
utumbo wakati karoti na hummus unayapa macho yako ulinzi.
Wataalamu wa lishe wanasema hakuna mchanganyiko
utakaoyeyusha mafuta au kubadili uzee - lakini ulinganifu mzuri wa chakula, unaweza
kusaidia mwili wako kufyonza virutubisho kwa urahisi na kukufanya mwenye afya
zaidi wakati wote bila kujali umri wako.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni